Mambo yamezua jambo ambapo wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu inayokutana hivi sasa chini Rais Dkt Jakaya Kikwete wameonesha wazi kupinga uamuzi wa mbunge wa Monduli Edward Lowassa jina lake kukatwa.
Hayo yamedhihirika hivi sasa wakati Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt Jakaya Kikwete akiingia kufungua mkutano huo ambapo imezoeleka wajumbe huimba kuwa na imani na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dkt Jakaya Kikwete lakini leo hali imekuwa tofauti. Wajumbe walipaza sauti zao wakiimba wimbo wa kuwa na imani na Edward Lowassa.( Tuna Imani na Lowassa...!!! Tuna Imani na Lowassa!!)
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa walio omba ridhaa ya kuteuliwa kugombea urais ndani ya chama hicho.
Huku hali ikiwa si shwari ndani ya CCM baada ya kukatwa majina makubwa kama ya akina Lowassa , imeibuka hii ya fedha kukamatwa hotelini zikidaiwa kupelekwa na miongoni mwa watangaza nia ya urais ili kuwapa wajumbe wa NEC
Kuhusu taarifa za kijana aliyenaswa na masanduku ya fedha upekuzi bado unaendelea kwenye eneo la tukio ambo taarifa zisiso rasmi zinadai kuwa kijana huyo alikamatwa na wafuasi wa Mh.LOWASSA ambao waliweza kuripoti Polisi na Takukuru na inadaiwa kuwa fedha hizo zilipelekwa kwa ajili ya kugawia wajumbe waweze kumchagua mmoja wa wagombea.
Ni katika St. Gasper Hotel ambapo ilikuwa ni kambi ya Edward Lowassa sasa hivi zimekamatwa fedha zinazodaiwa kuandaliwa kugawiwa kwa wajumbe wa NEC.
Aliyekamatwa kageuka, anasema katumwa na Membe
Taarifa zaidi tutawafahamisha kadiri zitakavyo thibitishwa na mamlaka zinazoendelea na Uchunguzi.
Wakati huo huo
kuhusu taarifa zilizoenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambaye amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika ujumbe @Twitter kukanusha kuhusika na mtu huyo
“Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna “Mtu wa Membe” amekamatwa na pesa Dodoma“
Kwenye Tweet nyingine Waziri Membe ameandika hivi
”siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu” @BernardMembe
Social Plugin