Majambazi wanne waliokuwa wamejificha katika ziwa Buligi wilayani Karagwe mkoani Kagera kwa lengo la kutekeleza vitendo vya uharifu huku wakiwa na silaha mbalimbali za kivita wameuwawa na jeshi la polisi mkoani Kagera wakati wakijiandaa kuvamia na kupora mali za wananchi katika mapambano ya kujibizana lisasi na jeshi hilo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika tano.
Akiongea mara baada ya tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Augastine Leone Ollomi amesema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema juu ya ujio wa majambazi hao ambao walikuwa wamejificha katika ziwa Buligi huku wakijiandaa kwenda kufanya matukio ya uharifu katika kijiji cha Bisheshe wilayani Karagwe na kwamba majambazi hao walianza kujibizana risasi na jeshi la polisi na kufaniwa kuwauwa majambazi wanne na katika tukio hilo hakuna askari yeyote aliye jeruhiwa.
Kamanda Ollomi ameongeza kwa kusema mkoa wa Kagera sasa unakabiliwa na matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya watu kukatwa kolomeo na matukio ya majambazi ambayo yameanza kujirudia ambapo ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa ujumla kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona viashiria vya watu wasio wawema wanaopanga njama za kufanya matukio ya kiuharifu ili kwapamoja waze kudhibiti matukio hao yanayojitokeza mara kwa mara katika mkoa huo.
Via>>ITV
Social Plugin