Shirikisho la soka Nigeria NFF baada ya
kupitiwa taarifa za Kamati ya Nidhamu, Ufundi na Maendeleo. limefikia
uamuzi wa kumtimua kazi kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Super Eagles’, Steven Keshi kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Makamu wa kwanza wa Rais wa NFF, Seyi Akinwunmi amewahakikishia Wanigeria kwamba uamuzi huo haujachukuliwa kwa kukurupuka, bali umezingatia maslahi ya soka ya Nigeria.
Keshi, ambaye ni Nahodha wa zamani Super
Eagles amekuwa kocha wa timu ya taifa kwa vipindi vitatu tofauti kati
ya mwaka 2011 na 2015, na mafanikio yake makubwa yakiwa ni kuwapa Kombe
la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 Afrika Kusini na kufika Raundi ya Pili
katika Kombe la Dunia mwaka jana Brazil.
Kocha huyo amefukuzwai ikiwa ni miezi
miwili kabla ya Nigeria kusafiri kuja Tanzania kumenyana na Taifa Stars
katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka
2017.