Habari zilizotufikia usiku huu inasemekana kuwa kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Dodoma kimepitisha majina matano ya watia nia ya Urais nchini Tanzania kupitia CCM.
Majina yanayotajwa sana ni:
Asha Rose Migiro,Bernard Membe,John Magufuli,Januari Makamba na Amina Salum Ally
Mwandishi wa habari Dotto Bulendu aliyeko eneo la Tukio..anasema
"Mpasuko CCM,Kamati kuu imemaliza kazi yake muda huu,Nape amesema hawawezi kutangaza majina matano yaliyopita,huku Dr Emmanuel Nchimbi,Adam Kimbisa na Sofia Simba,wakisema hawakubaliani na maamuzi ya kamati kuu,inadaiwa yamepitishwa majina matatu tu kati ya 38,Nape anasema majina hayo yatajadiliwa kesho,Nchimbi anasema wagombea wanaokubalika sana wamekatwa".
Social Plugin