LOWASSA AKARIBISHWA RASMI UKAWA,AAHIDIWA USHIRIKIANO WA HALI YA JUU
Monday, July 27, 2015
Hatimaye umoja wa katiba ya wananchi Ukawa umemualika rasmi mbunge wa Munduli kwa tiketi ya CCM Bw Edward Lowasa kujiunga na umoja huo na kwamba utahakikisha wanashirikiana naye kikamilifu.
Ni mwanzo wa wiki ambao kila mtanzania alikuwa akisubiri kusikia kitakachojili katika mkutano kati ya viongozi wa ngazi ya juu wa Ukawa na waadhishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya picha kadhaa kuonekana katika mitandao ya kijamii, sasa huenda ikawa ni rasmi.
Viongozi hawa wanasema wamefikia uamuzi huo kwa kile walichokiita ni uonevu, hadaa, udhalilishaji, upendeleo na ukandamizaji katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, na kwamba wametafakari kwa kina na kuona wanatakiwa kuwa na mgombea mwenye sifa na ueledi katika kulinda, kuheshimu, na kusimamia rasilimali za nchi.
Baadhi ya vigogo hao wa siasa kwa nyakati tofauti waliwahi kusikika wakimtaja Bw Edward Lowasa kuwa ni fisadi baada ya kukumbwa na kashifa kadhaa zikiwemo za Richimond, lakini kwa sasa wanasema yaliyopita si ndwere tugange yajayo.
Hata hivyo habari za ndani na za kuamini ndani ya Ukawa zinasema kuwa mbunge huyo wa Munduli anatarajiwa kujiunga na moja ya chama ndani ya umoja huo muda wowote kuanzia hivi sasa. Mbatia: Tunamkaribisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward Ngoyaye Lowasa kujiunga na UKAWA, ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.
Mbatia: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri
Lipumba: "Lowasa alishasema yeyote mwenye ushahidi aulete..hapa tumekaribisha Watanzania wote kujiunga. Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin