Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MANENO MAZITO YALIYOZUNGUMZWA NA WALIOBURUZWA NA MAGUFULI KWENYE TATU BORA...BAADA YA MAGUFULI KUPATA USHINDI MNONO

Mwenyekiti wa CCM taifa,Rais Jakaya Kikwete ameanza kwa kumkaribisha Mgombea aliyechukua nafasi ya Tatu katika Tatu bora, Dkt Asha Rose Migiro kwa ajili ya kutoa neno katika mkutano mkuu wa CCM Dodoma 2015

Dkt Asha Rose Migiro-"Mimi nilibahatika kuwa mmoja wa waliobahatika kuingia kwenye listi ya wanawake wawili shupavu kufanikiwa kuingia tatu bora,Niwapongeze pia wanaCCM wenzangu waliojitokeza kuwania nafasi ya urais,leo ni siku ya kihistoria,tunaanza kumsaka mtu atakayepeperusha bendera ya CCM"

"Mheshimiwa mwenyekiti naomba nitoe pongezi kwa Dkt John Magufuli kwa kufanikiwa kupata nafasi hii,nimpongeze mwenzangu Amina Salum kwa kushika nafasi ya pili,Huu ni mkubwa ,Magufuli amepata kura zinazostahili,wingi wa kura alizopata ndiyo utakuwa siri ya Ushindi wetu,kama kauli yetu inavyosema Umoja ni Ushindi,....Nitaungana na WanaCCM wenzangu  tutasimama pamoja katika kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi mkubwa" -- Dkt Asha Rose Migiro

"Kwako Dkt Magufuli chama chetu naona chama kiko salama,Naamini utalinda Mapinduzi ya Zanzibar..nauona umadhubuti wa muungano wetu,umoja wa chama chetu.....Kutoka kwako Magufuli naamini utafanya vyema....Nakutakia uongozi wenye ufanisi kwenye taifa letu....."- Dkt Asha Rose Migiro

Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete anamkaribisha mgombea mwingine aliyeingia kwenye Tatu Bora...Balozi Amina Salum Ally

Balozi Amina Salum Ally"Heshima niliyopewa ni kubwa sana licha ya kura kutokuwa nyingi,nitauenzi uanachama wangu,nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu katika chama changu,Naomba kuwahakikishia wenzangu kuwa nitakisimamia vyema chama changu kwa kumuunga mkono ndugu Magufuli,ili chama kipate ushindi mnono,nitaendelea kuchangia katika kudumisha mambo yote mazuri ya CCM....."

"Mshimiwa mwenyekiti,mchakato huu unaonesha kuwa chama kina utajiri wenye uwezo wa kuongoza nchi....Wanawake tumejadiliwa kwa haki sawa na wanaume,CCM imeandika historia kwa kuwapa nafasi kubwa wanawake...Kaka yetu,mpendwa wetu atatulea sisi wanawake tuweze kufika mahali juu zaidi....Nitakuwa mstari wa mbele kumuunga mkono ndugu yangu Magufuli....naamini kwamba CHAMA kwanza,MTU baadaye,Magufuli ni mwenzetu tena ni mtu wa kawaida,ni mzalendo hana makuu....Nawahakikishieni kuwa atafanya mambo makubwa katika chama chetu,tumuungeni mkono"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com