MAWAZIRI WA MKAPA: BASILI MRAMBA NA DANIEL YONA WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU KWA KUITIA HASARA SERIKALI




Vilio simanzi na majozi vimetawala katika viunga wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam pale jopo la majaji watatu walipothibitisha pasipo na shaka kuwa Bw Basil Mramba na Bw Daniel Yona waliokuwa ni mawaziri wa serikali ya awamu ya pili wanapaswa kwenda jela kwa miaka mitatu na kulipa faini ya shilingi milioni tano kwa makosa yanaowakabili yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisasabisha serikali hasara. 


Katika mahakama hiyo ndugu wawashtakiwa hao walionekana kutoyaamini yale yanayotokea na wengine kujikuta wakitiririkwa na machozi ambapo wakati hao wakiwa katika hali hiyo ndugu wa upande wa aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha Bw.Gray Mgonja ambaye na yeye alikuwa ni miongoni mwa washtakiwa walijikuta wanapigwa na butwaa baada ya ndugu yao kuachiwa huru na mahakama hiyo baada ya kutokutwa na hatia yoyote.

Bw.Mgonja ambaye muda mwingi alionekna kusimama tuu bila ya kuzungumza chochote alijikuta anaishia na maneno ya kukiambia kituo hiki pale alipotakiwa kusema lolote zaidi ya kusema hayo yote amemwachia mungu na yamefanyika kwa rehema za mungu.

Awali wakili wa serikali Tumaniel Kweka amesema Bw Mramba amekutwa na makosa kumi na moja isipokuwa Yona ambaye makosa yake ni pungufu ya hapa na kwamba watapaswa kulipa fidia ya shilingi milioni tano kwa kosa la kumi na moja na kama watashindwa kulipa watapaswa kwenda jela kwa mika mitatu ingwa bado watapaswa kwenda jela miaka mitatu kwa makosa hayo mengine.

Kwa upande wakili wa utetezi wamesema hawajaridhiswa na hukumu hiyo na hivyo watakata rufaa ndani ya kipindi kifupi kijacho itakumbukwa kuwa washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa kuwa walikuwa watumishi wa umma ambao Oktoba 30 mwaka 2003 walikaidi ushahuri wa mamlaka ya mapato Tanzania wa kuwataka wasitoe msamaha kwa kodi kwa kampuni ya Alex Sterwart hatua ambayo iliisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post