MREMBO AFARIKI DUNIA AKIPIGA PICHA JUU YA DARAJA ILI AVUNJE REKODI
Tuesday, July 07, 2015
Upigaji wa picha za selfie bado umeendelea kupata umaarufu katika sehemu mbalimbali duniania kutokana na teknolojia ya mitandano ya kijamii kuendelea kukua kwa kasi.
Matukio ya watu kupoteza maisha wakati wakitaka kupiga selfie za kipekee imekua ikitokea kila wakati lakini watumiaji bado wanashindwa kuwa makini.
Stori ya leo inatokea huko Russia ambapo msichana mmoja amepoteza maisha wakati akipiga selfie na wenzake juu ya daraja maarufu lililopo eneo la Moscow International Business Center.
Uchunguzi wa polisi umesema tukio hilo lilitokea siku ya jumamosi ambapo msichana huyo akiwa na rafiki zake walianza kupiga picha juu ya daraja hilo bila kuchukua tahadhari na ndipo upande wa daraja hilo ulikatika na mmoja wao kudondoka na kupoteza maisha.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin