Leonard Derefa enzi za uhai wake
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM mwaka 1995 hadi 2005 Leonard Derefa amefariki dunia leo asubuhi kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu muda mfupi baada ya kutoka uwani kujisaidia.
Leonard
Derefa( Mwanaderefa) alizaliwa mwaka 1942 katika kijiji cha Bulima wilaya ya Misungwi mkoani
Mwanza na hadi umauti unamfika alikuwa anaishi katika mtaa wa Mbuyuni kata ya
Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mmoja wa watoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Newe Derefa amesema
baba yake alifikwa na umauti leo saa 12 asubuhi muda mfupi baada
ya kutoka uwani kujisaidia.
Newe
amesema kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mama yake, Thereza Derefa mara
baada ya mumewe kutoka uwani aliingia chumbani na badala ya kurejea kitandani
alipiga magoti pembezoni mwa kitandani na kuanza kusali huku akitoka jasho jingi mwilini kiasi cha kulowana.
Amesema mama aliamua kumgusa na kumsemesha mume wake ili kujua kitu gani kilichomsibu lakini hakujibu chochote ndipo akatoa taarifa kwake(Newe) juu ya hali ya mzee..
Amesema mama aliamua kumgusa na kumsemesha mume wake ili kujua kitu gani kilichomsibu lakini hakujibu chochote ndipo akatoa taarifa kwake(Newe) juu ya hali ya mzee..
"Kufuatia hali hiyo tulimchukua na kumpeleka katika hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, madaktari walimpima ili kuelewa tatizo lakini walibaini
tayari ameishafariki dunia”,amesema Newe.
Kufuatia
taarifa za kifo hicho Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga kimetoa
salaam za rambirambi kwa familia ya marehemu,wanashinyanga, na kueleza jinsi
kilivyoguswa na msiba huo na kwamba marehemu alikuwa mwanachama mwadilifu
wa chama na ameacha pengo kubwa kutokana na jinsi alivyokuwa akitegemewa na
chama kwa ushauri mbalimbali.
Akizungumza
na Malunde1 blog, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Khamis Mgeja amesema Mzee Derefa
alikuwa mwanachama mchapakazi,mwaminifu, mwadilifu na mshauri mzuri wa chama na jamii kwa ujumla.
“Msiba
huu umetugusa sana,kwani mzee Derefa amekuwa kiongozi wa muda mrefu,amekuwa
Mbunge,kiongozi wa vyama vya Ushirika,amelitumikia taifa kwa uhodari
mkubwa,uaminifu na uadilifu mkubwa kwa ushirikiano mkubwa sana na
wenzake”,ameeleza Mgeja.
Tangu Tanzania
ipate uhuru, Jimbo la Shinyanga Mjini limeongozwa na wabunge tisa ambao ni John
Rupia, Bakari Msonde, Anna Tito Kachima, Ntemi Nyanda, Haninghton Mfaume, Paul
Makune, Leonard Derefa, Dk Charles Mlingwa na sasa Stephen Masele.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin