Gari aina ya Hiace iliyogongwa kwa nyumba na Fuso na kuuwa watu huko Moshi
Gari aina ya Hiace iliyogongwa kwa nyumba na Fuso na kuuwa watu huko Moshi
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 11 wamejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya hiace waliyokuwa wakisafiria kugongwa na fuso katika eneo la mto Kikavu wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Fulgence Ngonyani amesema ajali hiyo imetokea mapema leo baada ya Fuso hilo ambalo lilikuwa nyuma ya hiace hiyo zote zikielekea mjini Moshi kuongeza kasi katika mteremko huo na kugonga gari hilo la abiria kwa nyuma.
Kamanda Ngonyani amesema Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai, na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya mkoa Mawenzi na wengine katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi.
Kamanda Ngonyani amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Fuso hilo, na kwamba dereva wa Fuso hilo amekimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo.
Muonekano wa hiace baada ya ajali
Eneo la tukio
Lori lililosababisha ajali
eneo la tukio
Social Plugin