Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), imemaliza kikao chake cha kuteua majina matatu ya watia nia ya kuwania urais yatakayopelekwa katika Mkutano Mkuu, saa tatu usiku wa leo.
Waliopitishwa ni Dkt John Magufuli, Dkt Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali.
Mmoja kati ya hawa watatu atapigiwa kura na mkutano mkuu leo kupeperusha bendera ya CCM ya Katika uchaguzi Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,
wagombea walioachwa Bernard Membe na January Makamba wamekubali na
kuyapokea matokeo na kusema kuwa wako tayari kumuunga mkono mgombea
yoyote atakayechaguliwa na mkutano mkuu.
Social Plugin