Kumekuwa na story mfululizo toka ndani ya Kikao cha Bunge, Dodoma
kwamuda wa siku tatu mfululizo zimetokea vurugu, Kikao kimeahirishwa kwa
siku mbili mfululizo.
Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge
lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu kwa siku moja
ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika
AnneMakinda akaahirisha Bunge.
Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George
Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa
kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda
akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni
kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.
Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel
Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko
kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia
asiingie kwenye Kikao?
Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena
kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa
kuhudhuria Vikao vya Bunge kwasiku tano kila mmoja.
Ezekiel Wenje
Mussa Kombo
Masoud Abdallah Salim
Rebecca Ngodo
Sabrina Sungura
Khatib Said Haji
Dr. Anthony Mbassa
Maulidah Anna Valerian Komu
Kulikoyela Kahigi
Cecilia Pareso
Joyce Mukya
Mariam Msabaha
Grace Kiwelu
Israel Natse
Mustapha Akonaay
Konchesta Rwamlaza
Suleiman Bungura
Rashid Ali Abdallah
Ali Hamad
Riziki Juma
Rukia Kassim Ahmed
Azza Hamad
Khatibu Said Haji
Kombo Khamis Kombo
Ali Khamis Seif
Haroub Mohammed Shamisi
Kuruthum Jumanne
Mchuchuli
Amina Mwidau
Mkiwa Kimwanga
Salum Baruhani
Marry Stellah Malaki
Rashid Ally Omary
Mwanamrisho Abama
Lucy Owenya
Nje ya ukumbi wa bunge wabunge hao waliotolewa nje wakazungumza na
waandishi wa habari wakaelezea kitendo cha wao kutolewa nje pamoja na
sababu za wao kuikataa miswada hiyo kuletwa yote pamoja na kwa hati ya
dharura.
Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo
ni sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi
pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji
Tanzania ambapo akiwasilisha muswada wa petroli bungeni mjini dodoma
waziri wa nishati na madini Mh.Simba Chawene amesema mswada huo utajenga
mfumo imara wa kusimamia sekta ya mafuta na gesi.
Wenyeviti wa kamati hizo nao wakawasilisha maoni na ushauri wa
kamati zao ambapo mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini Mh. Richard
Ndassa akisoma mani ya kamati amesema kamati imekubalina na serikali
kuhusu mamlaka aliyopewa waziri pamoja na maoni ya wadau kuhusu
kumuongezea waziri mamlaka kisheria kuingia mikataba mikubwa ya miradi
ya gesi asilia pasipo kuingilia au kuwa na mamlaka sawa na TPDC.