Kikao
cha Bunge kilianza kama kawaida jana July 02 2015, baada ya kipindi cha
maswali na majibu yaliyoulizwa kwa Mawaziri, Mbunge John Mnyika akaomba
mwongozo.
“Tumekabidhiwa orodha ya
shughuli za leo.. kimsingi imekiuka kanuni, uamuzi wa kuileta hii
miswada mitatu kwa pamoja kama hati ya dharura umekiuka kabisa msingi wa
makubaliano ya kwenye Semina ambapo Wabunge kwa kauli moja tulikataa
Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharura“
“Naomba Mwongozo, hili jambo linahitaji majibu sasa” >>> Mbunge John Mnyika.
Spika Makinda akaanza
kutoa ufafanuzi kuhusu hiyo ishu >>> “Toa kwanza maneno ya
kuniamrisha mimi cha kufanya… Hakuna mtu anayeweza kuniamrisha”
>>> Anne Makinda.
Spika akaendelea
>>> “Tumefanya mara nyingi sana wala sio leo tu, hakuna kanuni
iliyovunjwa na sio mara ya kwanza kujadili kitu kinachofanana kwa
pamoja”>>> Spika Anne Makinda.
Hakukuwa
na suluhu ya hilo, Wabunge wa Upinzani wakagomea Mjadala huo kuendelea
ikabidi Kikao cha Bunge kiahirishwe saa nne asubuhi.
Angalia Video Hapa:
Social Plugin