Noma Sana!! BABA AAMUA KUKATA VIDOLE VYA MWANAE KWA KISU,KISA KAIBA NYAMA....
Sunday, July 05, 2015
Matukio ya wazazi kunyanyasa watoto tena hata wa kuwazaa wenyewe bado yameendelea kutokea kila wakati sehemu mbalimbali duniani.
Huko Nigeria kuna stori inamuhusu baba mmoja..eti kaamua kukata vidole vya mwanae wa kumzaa kisa tu kaiba nyama bila kumwomba mama yake ruhusa ya kuchukua.
Hata hivyo polisi hawakumuachia baba huyo aitwaye Surulere Rafael kwa kumfungulia mashtaka na alipoulizwa sababu ya kumkata mwanaye huyo alisema alimwibia fedha kiasi cha zaidi ya 10,000 za Kitanzania pia aliiba mboga bila kuomba na kuamua kumpa adhabu hiyo.
Kwa sasa mtoto huyo amelazwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu wakati baba yake akiendelea kushikiliwa na polisi.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin