Baadhi ya vitu vilivyokutwa juu ya kaburi la Marehemu
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo
Wakazi wa eneo hilo wakishangaa mizigo hiyo
Katika tukio lisilokuwa la kawaida ambalo limevuta umati mkubwa wa watu katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu katika eneo la makaburi ya Kidinda ni wananchi kukuta kwenye kaburi moja wapo kukiwa na vitu mbalimbali ikiwemo godoro,mabegi,viti,kitanda,meza,vyombo na thamani mbalimbali za ndani.
Mashuhuda waliobaini kuwepo kwa tukio hilo wamesema inawezekana linatokana na imani za kishirikina.
Wamesema walifika katika makaburi hayo kwa ajili ya kumsitiri ndugu yao aliyefariki lakini cha kushangaza wakaona juu ya moja ya makaburi kukiwa na vitu hivyo na kudai kuwa huenda marehemu alizikwa navyo.
"Sisi tulikuwa na msiba wetu..tukaja hapa makaburini kumzika ndugu yetu, ghafla tukaona juu ya kaburi jingine kuna vitu hivyo..inaonekana huyu marehemu alizikwa na vitu vyake vikaletwa hapa makaburini na kuwekwa juu ya kaburi lake",ameeleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus Rweyemamu.
Kufuatia taarifa hizo waandishi wa habari ikiwemo Malunde1 blog bila kupoteza muda walifika katika eneo la tukio na kukuta vitu hivyo vikiwa juu ya kaburi la marehemu, huku wahusika waliofanya hivyo wakiwa hawajulikani kutokana na wahusika wa msiba kutokujulikana.
Hata hivyo baada ya askari polisi kufika eneo la tukio walivichukua vitu hivyo na kuondoka navyo kituo cha polisi Bariadi .
Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba wanaendeela kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Social Plugin