Busu
Busu la wanyama
Busu
Utafiti mpya umegundua kwamba busu la mdomo kwa mdomo sio ishara kamili ya kuonyesha mapenzi, kinyume na dhana ya watu wengi
Aidha wanyama wa porini pia wameonekana kutojali mtindo huo.
Swali ni je busu kama ishara ya mahaba limeenea vipi kutoka kizazi kimoja hadi chengine?
Ukitizama tendo hilo la busu la mdomo kwa mdomo kwa kina, si la kufurahisha sana, kuna kubadilishana mate, ambayo kwa wastani, yana bakteria zaidi ya milioni 80, na si wote wazuri
Lakini kwa hakika kila mtu anayeshiriki tendo hilo hukumbuka busu lake la kwanza kwa undani hata kama lilipendeza ama lilikuwa la kuaibisha, na kwa hivyo ni tendo ambalo linaendelea kuwa msingi wa kuashiria mahaba.
Katika jamii ambazo bado zimejikita katika mila na desturi, hakuna ushahidi wa chanzo cha busu kama ishara ya mahaba.
Kwa mfano katika jamii ya Mehinaku nchini brazil, wanachukulia kubusu kama kitendo cha uasi.
Kulingana na mwandishi William Jankowiak kutoka chuo kikuu cha Nevada, Las Vegas Marekani, utafiti unatofautiana na imani kwamba kubusu kunaonyesha mahaba kama dhana ya watu wengi duniani, na anasema ni ubunifu wa jamii ya wazungu unaopitishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi chengine.
Ushahidi wa kwamza kabisa wa mila ya kubusu ulinukuliwa kwa mara ya kwanza katika maandiko ya kihindi Vedic Sanskrit miaka 3,500 iliyopita na ilikuwa ishara ya kurithi nafsi ya mtu mwingine.
Ushahidi wa zamani wa kubusu unatokana Hindu Vedic Sanskrit maandiko ya zaidi ya miaka 3,500 iliyopita.
Wanyama wa pori pia hutumia busu kwa ishara zingine. Sokwe hushiriki tendo hili kama ishara ya kupatikana kwa amani baada ya mvurugano.
Via>>>BBC
Social Plugin