Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 30 - MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA AKIZUNGUMZA NA WANAWAKE JIJINI DAR ES SALAAM


Wanawake kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika ukumbi wa Milenium Tower katika mkutano wa baraza la wanawake wa Chadema ambao mgeni rasm ni mgombea wa urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ambaye amewataka wanawake kushiriki ipasavyo katika kuleta mabadiliko.



Mheshimiwa Lowassa aliyeambatana na viongozi wa juu wa chama hicho amesema wanawake wana mchango mkubwa wa kufanikisha ndoto za watanzania za kupata mabadiliko ya kweli.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa UKAWA akiwemo mwenyekiti wa Chadema Mheshimiwa Freeman Mbowe amewataka viongozi wa UKAWA kote nchini kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa nafasi ya kutoa mchango wao ipasavyo.

Awali mke wa mgombea urais kupitia UKAWA mama Regna Lowassa(pichani) amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kupokea mabadiliko sambamba na kujitokeza kupiga kura na kuhakikisha mabadiliko yanapatikana kwa amani na yanasaidia kupunguza makali ya maisha.












































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com