Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MHESHIMIWA LOWASSA AKIWA KWENYE DALADALA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM




Mgombea urais wa Chadema kupitia (UKAWA)Mh.Edward Lowasa ametembelea baadhi ya vituo vya mabasi vinavyotoa huduma katika jiji la Dar es Salam na vyenye kero kubwa kikiwemo cha Gongo la Mboto kwa lengo la kujionea adha ya usafiri wanayopata wananchi ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuondoa kero hiyo kama wananchi wakimchagua kuwa rais wa awamu ya Tano



 Lowasa aliyeambatana na mgombea mwenza Mh.Duni Haji baada ya kufika katika kituo hicho hakuishia tu kuwatazama wananchi wanavyotaabika na usafiri bali aliungana nao kusafiri kwa kutumia moja ya dala dala inayotoka Gongo la Mboto kwenda Kisarawe na kushuka Chamazi na kisha akatumia usafiri wa gari ndogo za abiria aina ya Noah kutoka Chamazi hadi Mbagala.

Licha ya kuwa ziara hiyo ilikuwa ni ya kushtukiza ilivuta umati mkubwa wa watu wa rika mbali mbali wengi wakiwa vijana ambao waliacha shughuli zao na kuanza kuwafuata viongozi hao wakitaka kusikia walau sauti zao na licha ya mgombea mwenza Mh.Duni Haji kuwatuliza kwa kuwaeleza kuwa watazungumza nao baada ya uzinduzi wa kampeni waliendelea kuwafuata viongozi hao.

Wananchi waliokuwa kwenye maeneo hayo wamesema hatua ya viongozi hao wa Ukawa ya kufika kujionea wao wenyewe taabu na shida zinazowakabili licha ya kuwapa matumaini ya kuondokana na tatizo hilo inadhihirisha adhima ya umoja wa ukawa ya kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa zaidi ya miaka hamsini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com