Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- SHIRIKA LA EFG LAFANYA KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABISHARA SOKONI SHINYANGA


Hapa ni katika Ukumbi wa Serengeti katika hotel ya Karena mjini Shinyanga ambako leo limeanza kufanyika kongamano la siku mbili la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni mkoani Shinyanga lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Equality For Growth (EFG) linalolenga kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwajengea uwezo wa kisheria na biashara wanawake walioko katika sekta isiyo rasmi nchini Tanzania.Kongamano hilo limeanza leo Agosti 25,2015 hadi kesho Agosti 26,2015.Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo alikuwa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Pudensiana Kihawa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Pudensiana Kihawa akifungua kongamano hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga


Mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Pudensiana Kihawa akizungumza katika kongamano hilo


Mkurugenzi mtendaji wa shirika la EFG Jane Magigita akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo amesema wameamua kuwakutanisha wanawake wanaofanya shughuli zao sokoni kwani mara nyingi wamekuwa wakisahaulika na kwamba asilimia 80 ya watanzania ni wajasiliamali ambao wapo kwenye sekta isiyo rasmi na wanaliingizia taifa kipato.

Kauli mbiu ya kongamano hilo lililokutanisha wanawake zaidi ya 100 ni " Kujenga msongamano wa wanawake katika sekta isiyo rasmi".Miongoni mwa malengo ya kongamano hilo ni kuwakutanisha pamoja wanawake wajasiriamali hasa wanaofanya shughuli zao sokoni,kutambulisha mradi wa EFG unaojulikana kwa jina la "Sauti ya Mwanamke Sokoni" na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu wanawake wafanyabiashara sokoni.


Shirika la EFG lilianzishwa mwaka 2008,na makao yake makuu yako jijini Dar es salaam


Wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara katika masoko mbalimbali mkoani Shinyanga


Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini.....


Kongamano linaendelea....


Kongamano linaendelea


Tunafuatilia kinachoendelea...


Kongamano linaendelea


Wajasiriamali wakiwa ukumbini


Kongamano linaendelea


Kongamano linaendelea


Waandishi wa habari nao walikuwepo wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo


Waandishi wa habari Nunu Abdul na Wezay Ally wakiwa ukumbini


Mwenyekiti wa sauti ya mwanamke soko kuu la manispaa ya Shinyanga Lydia Sheremia akizungumza katika kongamano hilo ambapo amesema wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingo wanapoendesha biashara zao ikiwa ni pamoja na lugha za matusi,benki kutowapa mikopo.


Washiriki wa kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja


Picha ya kumbukumbu


Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja


Picha ya pamoja


Washiriki wa kongamano hilo wakicheza ukumbini...baada ya wimbo "Wanawake na Maendeleo" kupigwa ukumbini


Wanawake wajasiriamali wakiserebuka ukumbini


Burudani ikiendelea ukumbini


Viongozi wa masoko yaliyopo katika manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini


Kongamano linaendelea
Afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga akiwa ukumbini

Msanii wa Bongo Movie Denice Sweya(Dino) akifanya yake ukumbini


Bi Edna kutoka EFG akiwa eneo la tukio

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com