ANGALIA PICHA VIGOGO WA CCM " WATIIFU" WA LOWASSA WAKIJIUNGA CHADEMA JIJINI DAR ES SALAAM
Tuesday, August 04, 2015
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kushoto) akimkabidhi kadi ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida ambaye ni Mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki Ndg.Mgana Msindai ambaye ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, kujiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA.
Msindai ni miongoni mwa wafuasi "watiifu" wa Mhe.Edward Lowassa. Inadaiwa wapo wenyeviti 15 wa CCM mikoa mbalimbali watajiunga na CHADEMA, baada ya Msindai kufungua njia.
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya chama hicho kwa Naibu Waziri wa Kazi Mh.Makongoro Mahanga.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Olemedeye akikabidhiwa kadi ya chama cha Chadema na Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kulia) akimkabidhi kadi ya CHADEMA, Mh. Isaya Simon Bukakiye, (katibu wa Uchumi na Fedha Wilaya ya Kahama CCM)
Chanzo-Mpekuzi blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin