Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA WAMPITISHA LOWASA KUWANIA URAIS KWA KISHINDO

Mkutano Mkuu wa chama cha upinzani cha Demokrasia na maendeleo Chadema, leo umempitisha Waziri mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kuwa mgombea wao wa urais na Juma Duni Haji kuwa mgombea mwenza .

Akitangaza uamuzi huo leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kukamilika kwa vikao vya ndani vya maamuzi vya chama hicho huku wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu wapigiga kura ya wazi ya kumpitisha wagombea hao.

Katika mkutano huo Chadema wamewapokea aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga, Mhe. Goodluck Ole Medeye pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa wenyeviti wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Mgana Msindai ambaye alizungumza kwa niaba ya wenzake.

Mfuasi wa Lowasa Mgana Msindai ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com