Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.
Mgeja akitangaza kuhamia Chadema
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa shinyanga ndugu Khamis Mgeja pamoja na kada maarufu wa chama hicho bwana John Guninita muda huu wametangaza Rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho kipo ndani ya UKAWA.
Katika mkutano unaoendelea baina ya makada hao wa CCM na wanahabari Jijini Dar es salaam wamesema kuwa wamechoka kuona chama kinatumia ubabe na mabavu kuwasimika watu ambao hawana uwezo wa kuiongoza hii nchi na kuacha viongozi wenye uwezo jambo ambalo wamesema hawawezi kulivumilia milele.
Akizungumza mwenyekiti huyo wa shinyanga Mgeja amesema kuwa chama cha Mapinduzi sasa huu ndio mwisho wake baada ya kukataa kufanya mabadiliko ndani ya chama chao jambo ambalo limewafanya watanzania kukichoka na kuitaji mabadiliko nje ya chama hicho.
'Mgeja ambaye alikuwa mfuasi wa Edward Lowasa amesema kuwa hali iliyotokea Dodoma katika mkutano wa kufanya uteuzi hali ya Mwenyekiti kuingia na majina yake matano mfukoni na kukataa ushauri wa viongozi na wanachama ni jambo ambalo lilionyesha udhaifu mkubwa ndani ya chama hicho hasa pale walipoamua kutumia silaha na vyombo vya usalama kuwatawanya wanachama waliokuwa wanaihitaji haki itendeke.
Akizungumzia mgombea wa Chama Cha Mapinduzi John Mgeja amesema kiongozi huyo ni sawa na Mwanafunzi (Learner) anayejifunza kuongoza nchi kwani hajawahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi kupitia chama hicho ,hivyo watanzania hawako tayari kuwajaribu watu katika nafasi kubwa kama ya Urais.
Mgeja amesema kuwa kama viongozi wa CCM wanahitaji kukijenga chama lazima watengue maamuzi hayo na kuwaomba radhi wanachama wa chama hicho na kisha kuchagua mtu ambaye anaweza kukivusha chama hicho tofauti na hapo chama hicho kinakwenda kufa.
Mgeja amesema kuwa kama wana CCM watahitaji mambo mengine waite mdahalo na viongozi hao wakaseme yale yote yaliyotokea Dodoma
Chanzo-habari24 blog
Social Plugin