Home habari HIZI NI BAADHI YA SENTENSI ZA LOWASSA LEO- SINA MSAMIATI WA KUSHINDWA..TUNACHUKUA DOLA ASUBUHI OKTOBA 25
HIZI NI BAADHI YA SENTENSI ZA LOWASSA LEO- SINA MSAMIATI WA KUSHINDWA..TUNACHUKUA DOLA ASUBUHI OKTOBA 25
Tuesday, August 04, 2015
Mkutano Mkuu wa chama cha upinzani cha Demokrasia na maendeleo Chadema, leo umempitisha Waziri mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kuwa mgombea wao wa urais na Juma Duni Haji kuwa mgombea mwenza,ziko hapa Baadhi ya sentensi za mheshimiwa Lowassa na Mbowe walizotamka kwenye mkutano huo.. Lowassa: Nataka nichukue fursa hii kuwapongeza wale wenzangu waliojiunga nami, maamuzi magumu lazima yafanyike. Lowassa: Watanzania wajue katika muungano huu tuna nguvu kubwa, nguvu ya kuweza kuchukua dola asubuhi Oktoba 25. 'alfajiri' Lowassa: Marafiki zangu na ndugu zangu mlioko Z'bar nawaambia hadharani kwamba nimejiunga na mtu ambaye havunji muungano Lowassa: Kwa watu ambao wamehangaika juu ya nchi hii ni viongozi wa dini, Gwajima, Kakobe na wengine asanteni sana. Lowassa: CHADEMA 'I came to join you for a reason; , kuwaondoa CCM madarakani Lowassa: Nataka kuwahaidi kuwa nitapita kila jimbo la nchi hii, kwahiyo unapoondoka hapa kajiandae katika jimbo lako. Lowassa: Niliwahi kuwaambia waandishi wa habari kwamba sina msamiati wa kushindwa Lowassa: Mchaka mchaka .....chinja... Aluta continue ..Nawashukuruni sana kwa kunisikiliza. Tutakutana kwenye majimbo. HIZI NI BAADHI YA SENTENSI ZA MHESHIMIWA MBOWE WOTE TULIAFIKIANA KUMPITISHA LOWASSA AKIWEMO KATIBU MKUU WA CHADEMA, DK SLAA- MBOWE Mbowe: Tunaamini tulianza na Mungu kwenye safari yetu, tunaimani tunaendelea na mungu na tutamaliza na mungu Mbowe: Tunaamini kila linalotokea ni mpango wa Mungu. Mbowe: Tumepigana kwa miaka 25 kufika hapa tulipo leo, haikuwa kitu rahisi, wapo waliopata matatizo mengi. Mbowe: Lakini wako tuliowaita magamba, nao wakaamua kimagamba magamba wakafunga safari yao ya matumaini kutafuta haki Mbowe: Tuna kila sababu ya kuwaunga mkono, tuna kila sababu ya kuwakaribisha kwetu ili ndoto hiyo itimie. Mbowe: Sisemi wanaokuja CHADEMA leo wote wana dhambi, hata sisi tulioko CHADEMA leo tuna mapungufu yetu. Mbowe: Kwahiyo nichukue fursa hii kumkaribisha Edward Lowassa, hawa ndio wenye chama chao sisi wengine wabeba dhamana tu Mbowe: Kwenye CHADEMA hakuna aliye mkubwa kuliko chama chetu, tukikubaliana tunasonga tunasonga tu. Mbowe:Yale mabaya mliyokuwa nayo kwenye chama chenu cha zamani tumeyasamehe, tunaomba mtuletee yale mazuri mliokuwa Mbowe: Hadi siku ya jana Mgombea Mwenza wa CHADEMA alikuwa Waziri Zanzibar lakini ameona ajiuzulu kujiunga na sisi. Mbowe: Kwa sababu tuna uhakika wa kukamata madaraka ya nchi hii, hiyo sheria tutaibadilisha 'faster' Mbowe: Naomba nimhakikishie Mh. Duni, yuko kwenye mikono salama na atafanya kazi kikamanda Mbowe: Ngoja nisome historia ya Edward Lowassa kwa kujidai kidogo, nifute jasho na ninywe maji. Mbowe: Mh. Lowassa amemuoa mama Regina Lowassa na kujaliwa kupata watoto watano. Mbowe: Mh. Lowassa ni shabiki mkubwa wa michezo na alikuwa mchezaji mkubwa wa mpira wa kikapu. 'basketball' Mbowe: Kamati kuu ilifanya utafiti tena ilifanya utafiti kwa vikao vingi mfululizo Mbowe: Tafiti zetu zilituambia kwamba Mh. Lowassa akipeperusha bendera yetu ndani ya UKAWA, ndoto ya Taifa hili inatimia. Mbowe: Wote tuliafikiana na kukubaliana kwamba tumpitishe Lowassa, akiwemo katibu Mkuu Dk. Slaa. Mbowe: Mapendekezo ya Baraza Kuu yamekubali LOWASSA na Haji Duni wapeperushe Bendera ya UKAWA kwenye Urais Mbowe: Tumependekeza Maalim Seif pekee wa chama cha CUF awe mgombea wa Urais Zanzibar akiwakilisha UKAWA.
Via>>EATV
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin