Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hot News!! POLISI KUZUIA MAANDAMANO YA LOWASSA LEO AGOSTI 10,2015 DAR ES SALAAM




Muda mfupi uliopita kupitia kituo cha ITV kwenye taarifa ambazo zimetolewa na kituo hicho zinasema kuwa Jeshi la Polisi Tanzania limekataza Maandamano ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa wakati akienda kuchukua fomu ya kugombea Urais.




Edward Lowassa leo anaenda kuchukua fomu ya ugombea Urais kwenye makao makuu ya NEC ambapo kwenye taarifa yake iliyotolewa na vyombo vya habari jana aliomba wanachama wa Ukawa kujiunga nae wakati wa kwenda kuchukua fomu hiyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kuwa UKAWA hawana taarifa zozote za zuio la maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu Mgombea wao wa Urais Mh. Edward Lowassa yanayoanzia ofisi za CUF hadi tume ya Uchaguzi (NEC).


Ameeleza kuwa hawajapata taarifa za zuio hilo kuanzia ofisi za CUF badala yake wataendelea na ratiba yao kama ilivyo pangwa.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi ,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayoanzia CHADEMA kwenda NEC na kurudi Chadema makao makuu kinondoni


Taarifa za hivi punde zinasema baada ya mazungumzo kati ya Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam na Viongozi wa UKAWA, hatimaye jeshi la Polisi limekubali na kuruhusu maandamano ya mgombea Urais CHADEMA Mh. Lowassa yaanzie ofisi za CUF Buguruni kwenda Tume ya uchaguzi 
(NEC).

ANGALIA PICHA NA TAARIFA ZAIDI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com