Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamefurika katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ujao wilaya ya Shinyanga hususani jimbo la Shinyanga Mjini.Mkutano huo umeongozwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ndugu Patrobas Katambi maarufu kwa jina la "Mzimu wa Shelembi".
Viongozi wengine machachari waliohudhuria mkutano huo ni mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Kahama mjini mheshimiwa James Lembeli,mgombea ubunge jimbo la Kishapu Fred Mpendazoe na mgombea ubunge jimbo la Msalala kupitia Chadema ndugu Paul Malaika.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog Kadama Malunde, alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 38,Angalia hapa chini
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Makamanda wa Ukawa na wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa nzuri ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima wa CCM ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mkutano unaendelea
Mgombea ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku akisisitiza kuwa mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya kabila la CCM ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma Protas akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mjini James Lembeli akikaribishwa jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wakazi wa Shinyanga
Mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini mkoa wa Shinyanga wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Ukawa James Lembeli akiuzngumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kupuuza propaganda inayoenezwa kuwa mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli kuwa ni msukuma ili kuwarubuni watu wa kanda ya ziwa wampatie kura.
Lembeli alisema hakubaliani na propaganda kuwa Magufuli kuwa ni msukuma hivyo wasukuma wamuunge mkono kutokana na kutokuwa na msaada wowote kutetea haki za wasukuma akitoa kuwa wakati akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza dhambi na shida waliyopatiwa wafugaji wakiwemo wasukuma ambao waliuawa,waliteswa na kuibiwa mali zao ,Magufuli anayedaiwa kuwa ni Msukuma hakufungua mdomo wake kutetea wafugaji/wasukuma dhidi ya matatizo yaliyowakuta.
Wakazi wa Shinyanga wakimshangilia James Lembeli
Lembeli aliongeza kuwa kutokana na kitendo hicho cha kukaa kimya dhidi ya vitendo vya wafugaji hao inadhihirisha kuwa hayuko pamoja na wasukuma hivyo asionewe huruma bali watanzania wamchague Edward Lowassa ambaye ni jasiri na msema kweli.
Mheshimiwa James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa wakazi wa Shinyanga
Lembeli alitumia fursa hiyo kuwataka Wafuasi wa CCM wenye uchu wa kufanya mabadiliko na kiu ya maendeleo wahamie Ukawa mara moja kwani kuna watu ambao walikuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM wamefanya maamuzi akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga baada ya kuchoshwa na madudu ya CCM.
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Katambi alizungumzia pia sakata la kutekwa kwake kisha kuchaniwa fomu zake za ubunge sambamba na kufunguliwa mashtaka ya kupinga ubunge wake ambapo alisema alipambana kuhakikisha kuwa jimbo hilo haliendi CCM na atahakikisha kuwa CCM haishindi katika jimbo hilo
Katambi alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga kukubali mabadiliko na hata ikitokea akafariki wakati mapambano ya kuiondoa CCM madarakani yakiendelea wasikate tamaa wasonge mbele
Mkutano unaendelea
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa Ukawa/Chadema
Mgombea huyo wa ubunge wa Chadema katika jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi amewataka wanaShinyanga kushikamana na kuepuka vitendo vya usaliti na kuhakikisha kuwa wanawapa kura wagombea wa Ukawa badala ya kushangilia pekee kwenye mikutano.
Mkutano unaendelea
Kulia ni mgombea udiwani kata ya Shinyanga mjini atakayechuana na aliyekuwa meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukaam(CCM) akitambulishwa kwa wakazi wa Shinyanga
Mheshimiwa James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa umakini zaidi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Mkutano unaendelea
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas akizungumza katika mkutano huo
Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono baada ya kuulizwa kama wako tayari kuleta mabadiliko katika jimbo la Shinyanga mjini na nchi kwa ujumla
Katambi alisema tayari wasaliti wa Chadema wameshajulikana na kuapa kutokata tamaa katika kuwapigania haki wananchi huku akiwataka wakazi wa Shinyanga kumpa kura nyingi Lowassa,wabunge wa Ukawa na madiwani wote wa Ukawa
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Makamanda wa Ukawa wakifurahia jambo eneo la mkutano
Makamanda wa Ukawa wakiwa eneo la tukio
Katambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga leo ambpo alivitaja baadhi ya vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kilimo na ufugaji,viwanda,kupambana na umaskini,ujinga na malazi..
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Social Plugin