Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao idadi yao haikuwza kufahamika mara moja wamevamia kituo cha mafuta cha State Oil kilichopo eneo la Kisasa manispaa ya Dodoma na kuua walinzi wawili wa kituo hicho kisha kupora fedha taslimu shilingi milioni kumi na pamoja na vitu mbalimbali na kutokomea pasipo julikana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi David Misime amesema majambazi hayo yalivamia kituoni hapo usiku na kuwashambulia walinzi kwa kuwapiga na kitu kizito vichwani mpaka kupoteza maisha na kisha kuvunja kontena lililokuwa na shehena ya vifaa vya ujenzi na kuiba vitu mbalimbali pamoja na fedha taslimu shilingi milioni kumi.
Mwandishi wa habari hizi alifika kituoni hapo na kuzungumza na mashuhuda wa tukio hilo akiwemo meneja wa kituo hicho Anwar Saidi na mama ntilie aliyetambulika kwa jina la Sarah Siyao ambaye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kubaini tukio hilo.
Walinzi waliouawa kwenye tukio hilo wametambulika kwa majina ya Paulo Nduluma na Aloyce Patsango wote wakiwa ni jamii ya wamasai.
Kamanda Misime ameihamasisha jamii hasa wale wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu watambue kuwa uhalifu mwisho wake ni kuishia kwenye mikono ya dola.
Via>>ITV
Social Plugin