MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AANDALIWA MAKUNDI KABLA YA UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA UKAWA
Wednesday, August 26, 2015
Mgombea urais kupitia UKAWA Mh.Edward Lowassa anatarajia kuzungumza na makundi mbalimbali ya wanawake kabla ya uzinduzi wa kampeni kwa kueleza mipango alionayo katika kuinua uchumi wa wanawake na kupambana na umasikini.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Halima Mdee akizungumzana waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema Mh.Lowassa ambaye ataambatana na mkewe mama Regina Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali CHADEMA watazungumza na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wanawake katika ukumbi wa MILLENIUM TOWER saa nane mchana mkutano ambao pia utarushwa moja kwa moja na television ya ITV ambapo Mh.Lowassa atazungumza mikakati alionayo kwa wanawake na watoto na hatma ya maendeleo kwa taifa.
Aidha Mdee amesema Mh.Lowassa atapata fursa ya kuainisha kuhusu watoto wa kike wanaokosa fursa za elimu ,sekta ya kilimo ambayo inaajiri wanawake wengi pamoja na sekta ya afya ambapo pia Bawacha wamegawa kanda kumi kuhakikisha wanawafikia wanawake katika mikoa yote kupeleka ujumbe wa matumaini kwa wana wake kushiriki harakati za ukombozi kwa taifa lao.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin