Ofisi ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Chanzo-ITV
Social Plugin