Baada ya minongono ya kutaka kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa kile kilichodaiwa ni maelewano hasi na baadhi ya wakurugenzi wa chama hicho sasa ni rasmi,Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Lipumba amesema atabakia kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho kikongwe hapa nchini..
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.
Prof Lipumba aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 1999 kuhusu mchakato wa katiba amesema kwa sasa haoni kama UKAWA utafanikisha upatikanaji wa katiba bora itakayoweza kukidhi tunu za taifa, utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji.
Msomi huyo wa mashuhuri wa masuala ya uchumi nchini amesema katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi atajikita zaidi katika kuandaa ushauri wa mambo mbalimbali yanayopaswa kutekelezwa na serikali ijayo ambapo baada ya uchaguzi atajikita katika masuala ya kitafiti pekee.
Prof Ibarhimu Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari ambao hata hivyo haukuhusisha kiongozi yeyote wa chama cha wananchi CUF.
Social Plugin