Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini leo kimezindua rasmi kampeni zake za Uchaguzi mkuu ujao katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,ambapo wabunge wa majimbo yote ya Shinyanga wamehudhuria uzinduzi huo .
Uzinduzi huo umeongozwa na waziri wa Uchukuzi mheshimiwa Samweli Sitta na mbunge wa Mtella aliyemaliza muda wake Livingstone Lusinde ambao walitumia fursa hiyo kumnadi mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli na kumponda mheshimiwa Edward Lowassa wakidai kuwa hafai kuwa rais kutokana ufisadi wake na kwamba Ukawa wamekurupuka kwani hawamjui vizuri Lowassa.
Makada hao wa CCM pia walisema Lowassa hana lolote zaidi ya mbwembwe na visingizio vya hapa na pale-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Wanachama wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo
Mjumbe wa NEC taifa Gasper Kileo akizungumza katika mkutano huo ambazo aliwataka wanaccm kuwapuuza watu wanaozusha kuwa atahamia Chadema/Ukawa kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni rafiki yake na Lowassa,ambapo Kileo alisisitiza kuwa hajawahi na wala hafikiria kuhama CCM na kwamba CCM lazima ishinde katika uchaguzi mkuu ujao
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Mheshimiwa Samweli Sitta akizungumza katika mkutano huo,ambapo aliwatambulisha wagombea ubunge majimbo yote 6 ya uchaguzi mkoa wa Shinyanga ambayo ni Ushetu,Msalala,Kahama mjini,Kishapu,Shinyanga mjini,Kishapu na Solwa na kusisitiza kuwa lazima CCM ishinde katika majimbo hayo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal akiwasalimia wakazi wa Shinyanga na kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwani ndiyo watawaletea maendeleo
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuwapa kura wagombea wa CCM
Mgombea ubunge jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige akiwasalimia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Mgombea ubunge jimbo jipya la Ushetu mheshimiwa Elius Kwandikwa akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo ajigamba kuwa katika jimbo lake wameshamaliza kufanya uchaguzi wanachosubiri ni utaratibu tu tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Nchambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wanaShinyanga kuwapa kura wagombea wa CCM kwani ndiyo watakaowaletea maendeleo watanzania
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga kutochagua mbunge ambaye siyo mzawa wa Shinyanga na badala yake wampe yeye kura ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga huku akijisifu kuwa amefanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali kama vile afya,elimu,michezo n.k
Mheshimiwa Samweli Sitta akiwahutubia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo alisisitiza kuwa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa anahusika na sakata la Richmond na utajiri wake haueleweki
Msanii wa nyimbo za asili Madebe Jinasa akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini
Wafuasi wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM leo mjini Shinyanga
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alitumia muda mwingi kumponda mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa hasa kuhusu afya yake kwamba ni mgonjwa bila kutaja ugonjwa anaougua/anaoumwa
Mheshimiwa Lusinde akiwaombea kura wagombea wa CCM na kumpa sifa kem kem mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga
Tunafuatilia kinachoendelea hapa.....
Mheshimiwa Lusinde akiwa na wagombea ubunge majimbo yote ya Shinyanga,ambapo mmoja pekee wa jimbo la Solwa mheshimiwa Ahmed Salum hakuwepo kwenye mkutano huo kutokana na kuwa katika shughuli zingine za kichama
Wabunge watarajiwa majimbo ya Shinyanga wakiwa jukwaani
Wa tatu kutoka kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Kahama mjini mheshimiwa Jumanne Kishimba
Wanachama wa CCM wakicheza uwanjani
Baada ya mkutano kila mmoja akaendelea na shughuli zake wengine wakapanda kwenye magari yao kurudi makwao
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Wazee wa CCM wakiwa eneo la tukio
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Social Plugin