SOMA HAPA MAJINA YA WATAKAOGOMBEA UBUNGE CCM KATIKA MAJIMBO YALIYOBAKIA



Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kimeteua wagombea tisa wa nafasi ya ubunge katika majimbo ya uchaguzi tisa kati ya 11 yaliyorudia uchaguzi Agosti 13 mwaka huu huku mawaziri wengine watatu wakimwagwa.


Hatua hiyo ya CCM imefikiwa baada ya kamati kuu ambayo inaongozwa na mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya Kikwete kupitia na kujadili majina ya wagombea waliopita katika nafasi hiyo ambapo mawaziri walioshindwa kupenya kwenye kura za maoni na hata uteuzi wa kamati hiyo ni waziri wa mifugo na uvuvi, Dk. Titus Kamani, Busega waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Seif Rashid na waziri wa mazingira, Biligith Mahenge Makete.

Nape amesema majimbo mawili ya mkoani Singida na Manyara bado yanajadiliwa na kuhusu malalamiko ya wagombea, amesema yote yamefanyiwa kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za ngazi zote za chama na kwamba kura za maoni siyo kigezo pekee kuwania nafasi ya ubunge hivyo kuna taratibu kanuni za vikao mbalimbali vya chama, tathimini imefanywa na kusimamisha waliokidhi.

Wakati malalamiko yakiendelea dhidi ya wagombea walioshindwa na waliokatwa na chama hicho baadhi ya vijana wa chama hicho wamewataka watanzania na wanachama wa CCM kuendelea kuwa wamoja na mshikamano kwani mwezi Octoba siyo mbali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post