Hali ya taharuki na wasiwasi mkubwa umewakumba wanafunzi wa shule ya sekondari ya Selou katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,baada ya wanafunzi wa kike kukumbwa na ugonjwa usijulikana wa kutikisa vichwa bila kupumzika,kupiga kelele na kukimbia kimbia ovyo.
Ndivyo ugonjwa huu wa ajabu ulivyoibuka na kuwakumba wanafunzi wa kike katika shule hii ya sekondari Selou-Namtumbo mkoani Ruvuma.
Ni ugonjwa ambao huwalazimu wanafunzi hawa kutikisa kichwa bila kupumzika,kupiga kelele ambazo wakati mwingine ni kama zinaashiria maumivu hivi.
Na wakati mwingine wakikosa uangalizi wa karibu hukimbia ovyo kusikojulikana.
Wakati sintofahamu hii ikileta shida na kuumiza vichwa vya walimu wa shule ya Selou na kusababisha usumbufu darasani.
Lakini mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Selou,Bwana Benny John anasema tatizo hilo ambalo hutulia siku kadhaa na kuibuka tena limedumu kwa takribani mwezi mmoja na tayari wataalamu wa afya wa wilaya ya Namtumbo walifika shuleni hapo kufanya utabibu bila mafanikio.
Jitihada za kumpata mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuzungumzia hali hii zimegonga ukuta, lakini mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Bwana Ally Issa mpenyi anasema tatizo hilo lilianza kwa watoto wawili na baadaye kuenea kwa wanafunzi wengine na bado wanaendelea na uchunguzi.
via>>Itv
Social Plugin