Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MAALIM SEIF AIFARIJI FAMILIA ILIYOPOTEZA WATU 9 KWA KUTEKETEA KWA MOTO DAR ES SALAAM


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimsalimia na kumpa pole Bw. Massoud Matta aliyepoteza familia yake ya watu tisa akiwemo mkewe na watoto wake wanne kutokana na ajali ya moto iliyotokea Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimsalimia na mmoja wa wanafamilia ya Bw. Massoud Matta aliyepoteza familia yake ya watu tisa akiwemo mkewe na watoto wake wanne kutokana na ajali ya moto iliyotokea Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya kumfariji e Bw. Massoud Matta (wa pili kushoto) aliyepoteza familia yake ya watu tisa akiwemo mkewe na watoto wake wanne kutokana na ajali ya moto iliyotokea Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa nasaha kwa wanafamilia hao.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wananchi, katika eneo la Buguruni Mapipa, baada ya kumfariji Bw. Massoud Matta aliyepoteza familia yake ya watu tisa akiwemo mkewe na watoto wake wanne kutokana na ajali ya moto iliyotokea Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.

Nyumba ya Bw. Massoud Matta iliyoungua moto na kusababisha vifo vya watu tisa wa familia moja katika eneo la Buguruni Malapa Dar es Salaam. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Baba wa Familia iliyoteketea kwa moto (Masoud) amesema majina ya marehemu yalikuwa ni Samira Juma ambaye alikuwa mke wake. Ahmed Masoud, Aisha Masoud , Abilah masoud, Ashraf Masoud, hawa walikuwa watoto wake, mama yake mzazi, mfanyakazi wa ndani, na mwanamke aliyejukana kwa jina la Wadh hat akiwa na mtoto wake mdogo wa mwaka mmoja na nusu.
Baadhi ya picha zikionesha nyumba iliyoungua na sehemu waliyozikwa jana wale watu 9 wa familia moja wakiwemo watoto watano waliofariki kwa moto baada ya nyumba yao kuungua moto na wao kuungulia ndani eneo la Buguruni Malapa, Ilala jijini Dare es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com