WATU TISA WATEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM,ANGALIA PICHA HAPA
Thursday, August 27, 2015
Familia ya watu tisa imeteketea kwa moto katika tukio la moto uliotokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo eneo la Buguruni Malapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa majirani, walisikia kelele na walipoamka wakakuta moto mkubwa ukiwa unawaka katika nyumba hiyo.
Hata hivyo juhudi zao za kuvunja mlango ili kuokoa watu waliokuwamo ndani zilishindikana.
Mmoja wa mashuhuda amesema wamefanikiwa kutoa miili ya watu watano iliyoungua vibaya, na imedaiwa kuwa baba mwenye nyumba amenusurika kifo kutokana na kuwa kazini katika shifti ya usiku.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin