Mgombe urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameingia jijini Dar es Salaam kwa kishindo na kunadi sera katika jimbo la Kawe na Kibamba na amesema ameshakamilisha mipango na taratibu za kuondoa kero za watanzania anachosubiri ni ridhaa yao ya kumchagua kuwa rais ili aanze utekelezaji wa kuthibitisha ahadi zake kwa vitendo.
Aidha Mh Lowassa amesema akiwa rais atahakikisha kuwa wawekezaji wote wanaingia ubia na watanzania ili kuleta usawa wa kunufaika na rasilimali za nchina kuhusu wasiwasi wa kuibiwa kura amesema hilo haliwezekani kwani wapo vijana wa kutosha kulinda kura na ni jambo linalowezekana.
Awali mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe na baadhi ya wagombea ubunge akiwemo Halima Mdee wamewataka wananchi kupuuza njama za CCM za kuwasakama viongozi wa UKAWA na watanzania wengine wanaounga mkono mabadiliko.
Aliyekuwa waziri mkuu Mh Fredirick Sumaye ambaye kwa sasa amejuinga na UKAWA amewataka watanzania kutokatishwa tamaa na wanaoendelea kuwasakama wananchi wanaotumia haki yao ya kutaka mabadiliko kwani wanaongeza chachu ya mabadiliko.
Mchaka mchaka wa vuguvugu la mabadiliko unaoongozwa na Mh Lowassa viongozi wengine wa UKAWA unaelekea katika mkoa wa Morogoro.