Pikipiki za waendesha bodaboda wilaya ya Shinyanga zikiwa zimepaki nje ya ukumbi wa Ibanza Hotel mjini Shinyanga wakati wa kikao cha mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na waendesha bodaboda jana mjini Shinyanga kilichokuwa na lengo la kutoa elimu kwa wasafirishaji hao abiria ili kutambua faida za kujiunga na mifuko ya bima ya afya.Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog -Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania(NHIF) na waendesha bodaboda ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wasafirishaji hao wa abiria kwa njia ya pikipiki maarufu bodaboda, kujiunga na mifuko ya bima ya afya ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu hususani pale wanapopatwa na ajari.
Waendesha bodaboda wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini kubwa zaidi ikiwa ni kuhamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania(NHIF)
Mgeni rasmi/mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kutokana na asilimia kubwa wahanga wa ajari hapa nchini hivi sasa ni bodaboda ambapo imefikia hadi baadhi ya hospitali wameshawatengea wodi zao, na wengine wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa pesa za matibabu, hivyo ni vyema wakajiunga na mifuko hiyo ya bima ya afya ambayo itawasaida kugharamikia matibabu yote.
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na NHIF
Afisa uanachama kutoka (NHIF) mkoa wa Shinyanga Katoto Mohamed akielezea namna ya kujiunga na NHIF ,alisema kila mwendesha bodaboda atachangia shilingi 76,800 kwa mwaka mzima, ambapo pesa hiyo itagharamikia matibabu yote ,licha ya kutopatwa na ajari hata pale atakapougua malazi mengine.
Kikao kinaendelea
Afisa uanachama kutoka (NHIF) mkoa wa Shinyanga Katoto Mohamed akitoa maelezo namna ya kujiunga na NHIF
Afisa udhibiti ubora wa huduma NHIF mkoa wa Shinyanga Dkt Agostino Kisamo akitoa maelekezo juu ya faida ya kujiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya afya-NHIF
Afisa udhibiti ubora wa huduma NHIF mkoa wa Shinyanga Dkt Agostino Kisamo akitoa maelekezo juu ya faida ya kujiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya afya-NHIF
Waendesha bodaboda wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika ukumbi wa Ibanza Hotel
Kikao kinaendelea
Ofisa wa polisi kikosi cha Usalama Barabarani Koplo Kaijage akitoa takwimu za ajali zinazotokana na pikipiki mkoani Shinyanga
Waendesha bodaboda wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog -Shinyanga
Social Plugin