Mgombea urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amesema serikali yake itatilia mkazo suala la ukusanyaji wa kodi hasa kwa wawekezaji wa nje pamoja na kuangalia upya misamaha ya kodi ili kuiwezesha serikali kukusanya fedha nyingi zitakazosaidia kutoa huduma za kijamii kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
Dr John Pombe Magufuli ameyasema hayo katika uwanja wa amhuri uliopo mkoani Morogoro wakati akinadi sera zake kwa mamia kwa makumi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo amempongeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuongeza mapato ya serikali na kuongeza kuwa serikali yake itaongeza mapato ya serikali kwa kuangalia upya suala misamaha ya kodi kwa wawekezaji hususani wa kigeni.
Dr Magufuli ameongeza kuwa yeye si mwanasiasa mzuri bali ni mtendaji zaidi na kwamba baraza la mawaziri atakaloliunda litakuwa ni baraza la mawaziri la kuwatumikia wananchi kwa kutatua kero zao hasa wale wa hali ya chini na kuwataka watakaoteuliwa katika baraza lake wajipange.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania kuwa hawatajuta kumchagua Dr Magufuli kuwa rais wa awamu ya tano kwa kuwa ni mwadilifu na mzalendo na kwa kuchaguliwa kwa Dr Magufuli yeye rais Kikwete atapata usingizi mwema.
Dr Magufuli amefanya pia mikutano katika maeneo ya Ruaha, Mikumi, Kilosa na kisha Morogoro mjini ambapo baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kilosa Bwana Selemani Simba, katibu wa Chadema wilaya ya Kilosa Ibrahimu Selemani na katibu wa jimbo kilosa kati Bwana Musa Ngongi.
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi likimpokea mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni
Rais Kikwete akimnadi mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao.