ANGALIA PICHA-NEEMA YAIANGUKIA TIMU YA MPIRA WA PETE YA POLISI SHINYANGA,YAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KUTOKA MGODI WA DHAHABU WA ACACIA BUZWAGI




Hapa ni ndani ya ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ambako leo asubuhi Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ACACIA kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya mpira wa pete ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga vyenye thamani ya shilingi milioni sita inayoshiriki ligi kuu daraja la kwanza Tanzania.(Picha meneja wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Philbert Rweyemamu akikabidhi viatu)

Kulia ni meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Filbert Rweyemamu akikabidhi mpira kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha.Vifaa vilivyokabidhiwa na mgodi wa Buzwagi ni mipira minne , viatu pea/jozi 10,jezi za mipira 30 na track suti 14 



Kulia ni meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Filbert Rweyemamu akionesha moja ya jezi zilizotolewa na mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya timu ya Netball polisi Shinyanga inayoundwa na polisi na wananchi wa mkoa wa Shinyanga


Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya michezo,Rweyemamu amesema wamedhamiria kuinua mpira wa Pete mkoani Shinyanga na kuongeza kuwa lengo kuwasaidia wachezaji ili wafanye vizuri katika mchezo wa ligi kuu daraja la kwanza Tanzania bara unaotarajia kuanza wiki ijayo.


Rweyemamu amesema licha ya Mgodi huo kuifadhili Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga ambayo itashiriki kucheza msimu ujao wa ligi kuu bara ,Pia wamedhamilia kufufua mpira wa Pete kwa wanawake mkoani Shinyanga kwani michezo hivi sasa ni sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa vijana .


Zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo likiendelea






Meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Filbert Rweyemamu akishikana mkono na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha baada ya kukabidhi mipira minne , viatu jozi kumi,jezi za mipira 30 na track suti 14 kwa timu ya pete ya polisi mkoa wa Shinyanga 



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Kamugisha akizungumza baada ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo ambapo ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo kwani timu ya polisi ni miongoni mwa timu 24 zinazoshiriki ligi kuu daraja la kwanza na mchezo huo utaanza rasmi tarehe 19 na kuchezea katika viwanja vya Kambarage vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga.


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza.."Tunaishukuru kampuni ya ACACIA kwa nia yake nzuri ya kuinua vipaji vya michezo mkoani Shinyanga,lakini pia imekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwani licha ya kulisaidia jeshi la polisi vifaa vya michezo imekuwa ikitoa pia misaada ya ujenzi wa zahanati ,barabara,maabara katika shule za sekondari"





Kapteni wa timu ya Pete ya polisi mkoa wa Shinyanga Khadija Fatih, akizungumza ambapo amesema wamejiandaa vyema na mashindano hayo ya mpira wa Pete (Netball) taifa ambayo yataanza kutimua vumbi mkoani Shinyanga kuanzia Septemba 19 hadi Octoba 4, (2015) katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na kuahidi kutowaangusha Mashabiki wa Timu hiyo bali watarajie ushindi.


Wachezaji wa timu ya Netball polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa wameshikilia jezi zilizotolewa na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi


Picha ya pamoja baada ya makabidhiano,kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,wachezaji wa timu ya pete ya polisi na viongozi wa mgodi wa ACACIA Buzwagi







Picha ya pamoja


Picha ya pamoja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post