Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AUAWA AKIZUIA MIFUGO ISILE MAHINDI SHAMBANI KWAKE KILICHOFUATA NI STORI NYINGINE....




Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia wananchi wawili jamii ya wafugaji,kwa tuhuma za kumpiga hadi kumsababishia kifo mkazi wa Tindiga,tarafa ya Masanze wilayani Kilosa mkoani Morogoro,baada ya kujaribu kuwazuia wasilishie mifugo katika shamba lake la mahindi ambapo wananchi wenye hasira kali wamelipiza kwa kuwaua ng'ombe 68 kutokana na mauaji hayo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema mauaji ya mtu huyo,Said Sandali (42) mkazi wa Tindiga Kilosa, yametokea baada ya kujaribu kuwazuia wafugaji wasilishe mifugo kwenye shamba lake la mahindi,lakini wafugaji hao walimpiga hadi kusababisha kifo chake,jambo lililowatia hasira wana jamii wa eneo husika,ambao wamevamia ng’ombe 108 na kuwakata kata kwa mapanga, na kati yake 68 wakapoteza maisha.


Kufuatia tukio hilo kamanda huyo wa polisi ametoa wito kwa makundi ya wakulima na wafugaji kuheshimiana na kuacha kujichukulia sheria mikononi, na kuzishauri serikali za vijiji kushirikiana na watu wanaoheshimika na makundi yote kuunda sheria ndogo ndogo watakazozisimamia na kuzitekeleza,ambapo wananchi wametaka elimu ya uraia kuzidi kutolewa ili jamii ijitambue na wanasiasa kuacha kuwa chanzo cha uchochezi ili kuondoa matatizo kama hayo yanayojitokeza.


Tukio jingine limehusisha kukamatwa kwa vijana wawili kwa tuhuma za kufanya vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani,kwa kutembea usiku wakiwa wamebeba mfano wa majeneza yenye vitambaa vya kijani.

Via>>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com