TBS KUFANYA MSAKO MKALI NCHI NZIMA KUWABAINI WAUZAJI WA UMEME NURU 'SOLAR POWER PANELS' ZILIZO CHINI YA KIWANGO




Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi (katikati), akiwaonesha wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi Umeme Nuru (Solar Power panels) ambazo hazina ubora zilizokamatwa zikiwa katika soko la Tanzania baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi hiyo, kufanya uchunguzi na kubaini kuwepo katika soko solar hizo. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa Uhusiano, Roida Andusamile.




Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew, akiwaonesha wanahabari Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko ambazo ni bora.



Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu shirika hilo kuanza msako mkali wa kuwabaini wafanyabiashara wanaouza Umeme Nuru (Solar Power Panels), zilizochini ya kiwango. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi.



Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka,Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi, Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile.



Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe akizungumza katika mkutano huo.



Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.

SHIRIKA la viwango Tanzania limekuwa likifanya ukaguziwa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni na viwandani mara kwa mara, lengo likiwa niku hakikisha kuwa bidhaa hizo zinakidhi matakwa ya kiwango cha bidhaa husika wakatiwote. 

TBS kwakushirikiana naTaasisya NishatiJadididu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza kufuatia malalamiko mengi kuhusiana na ubora waVipande vyaumemenuru katika soko la Tanzania ilikutatuatatizo. Mnamo tarehe 23-06-2015, TBS ilifanya ukaguzi wa Umeme Nuru (Solar Power panels) katika maeneo yafuatayo; 


Keko- Mwanga, MtaawaMsimbazi, Mtaawa Congo.

TBS ilibaini baadhi ya wasambazaji walikuwa na bidhaa za umemenuru zilizo chini ya kiwangonyingizikitokeanchini China. 

Jumla ya vipande vya umemenuru 1321 kutokaduka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164 kutokaduka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya ubora wake kutiliwashaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka. Na vile vile wakaguzi walichukua sampuli kutokaduka la Keoali Power & EquipmentsCo.Ltd.

Matokeo ya maabara yalitoka na kuonesha kuwasampuli hizo zilizochukuli wakati kama duka tajwa zimefeli.

1. Vipande vya Umeme Nuru vinazosambazwa na Regal Solar Ltd vimefeli kufikia kiwango cha“marking and name plate”, kwa mfano hazijaonyesha nchi zinapotengenezewa,ainaya panel naserial namba; kipimo cha nguvu ya umeme inayotoka ni ndogo ukilinganishanakiwango cha chini cha nguvu ya umeme inayotakiwa kutoka, na hii ni kwa vipande vya umemenuru vilivyo na nguvu zifuatazo: 100W, 120W,70W,50W,20W,250W,30W,150W na 170W. 



2. Vipandevya Umeme Nuru vya Nishati Electronics Ltd vimefelikufikiakiwango cha “marking and name plate”,- havijaonyesha nchi zinapotengenezwa kipimo cha nguvu ya umemeinayotokanindogoukilinganishanakiwango cha chini cha nguvu ya umeme inayotakiwa kutoka ,hii ni kwa vipande vya umeme nuru vilivyo na nguvu zifuatazo: 100W,80W,70W,120W,40W,200W,30W. na kwa Vipande vya Umeme Nuru vya 120W na 200W kiwango cha juu cha mfumo wa nguvu ya umeme hakikubainishwa hivyo kukwamisha zoezi la upimaji.


3. Keoali Power &EquipmentsCo.Ltd vipande vya umeme nuru vimeonyesha kufeli “marking and name plate- havikuoneshanchizilipotengenezwa, ainayaplate, serial namba; havikubainisha kiasi cha juu cha mfumo wa nguvu ya umeme.

Tamko la Shirika


TBS inatoatamko kuwa zoezi hili niendelevu na iwapo msambazaji atabainika kukiuka na kuingiza bidhaa chini ya kiwango cha Afrika Mashariki EAS364:2005, Shirika litachukua hatua kali zakisheria.


Tunawasihi wafanyabiashara wanaouza bidhaa hafifu za vipandevya umemenuru kuziondoa madukani mara moja kablaShirika halijaanza zoezi hilo. 


Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao pindi bidhaa hizo hafifu zitakapokutwa madukani.


Vile vile tunapenda kuwafahamisha kuwa zoezi la kuondoa bidhaa hafifu sokoni ikiwa pamoja na nguo za ndani,vilainishi vya mitambo,juisi ( ready to drink) na mikate ya naendelea. Wananchi wasisite kuwasiliana nasi kupiti nanamba 0800 110 827 kwa kutumia mitandao ya TTCL na Vodacom bila gharama yoyote.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post