Mtoto Mary Emmanuel mwenye umri miaka mitano mkazi wa mtaa wa Kipika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekuwa akinyanyaswa kwa kunyimwa chakula na sasa amechomwa moto kiganja cha mkono wake wa kushoto na shangazi yake aitwaye Anneth Nyoku kwa madai ya kuiba kipande cha nyama.
Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Bi.Davina Maketa amesema mtoto huyo anadaiwa kunyanyaswa kwa kunyimwa chakula na kupigwa na shangazi yake anayeishi naye aitwaye Aneth Nyoku anayedaiwa kumchoma moto mtoto huyo huku wananchi wakilaani ukatili huo.
Naye mtuhumiwa wa ukatili huo Bi.Anneth Nyoku amesema hakuwa na nia mbaya kumchoma moto mtoto huyo bali lengo ilikuwa ni kumuonya kuacha tabia ya wizi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Revocatus Malimi amesema taarifa za tukio hilo bado halijafika mezani kwake na atalifuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyo.
Social Plugin