Watu wawili wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa kutokana na mkanyagano uliotokea jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Tayari leo, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewatembelea majeruhi hao waliolazwa Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19 waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia vibaya.
Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.
Dk Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Abdalah.
Uwanja wa Jamhuri jana ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.
Mara tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.
Angalia mafuriko menyewe hapa chini
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
Sehemu ya gharika la wananchi likimpokea mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni
Rais Kikwete akimnadi mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao.