HIKI NDIYO CHAMA CHA SIASA KILICHOFUTWA TANZANIA, HAKUNA KUFANYA KAMPENI ZA UCHAGUZI 2015


Msajili Msaidizi wa ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuufahamisha ummakuwa chama cha siasa Tanzania Peoples Party (TPP) kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa hapa nchini na chama hicho hakipo kwenye orodha ya vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini .Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali watu Emmanule Kayuni,.

Wanahabari wakimsikilza kwa makini Msajili Msaidizi wa ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza leo Jiji Dar es Salaam.
(Picha na Emmanue Massaka).

*******
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema kuwa Chama cha Tanzania People’s Party (TPP) kilifutwa, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutumia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema kuwa hivi karibuni kuna watu wameonekana katika chombo cha habari kimoja sio Michuzi, wakiwajinasibu katika chama cha TPP wakati chama hicho kilishafutwa toka 2001.

Nyahoza amesema kuwa watu wanaotumia chama hicho sheria itashika mkondo wake kwa kuwachukulia hatua watu kutumia chama ambacho kilishafutiwa usajili wa kudumu kwa msajili wa vyama vya siasa.

Aidha amesema kuwa vyama vilivyo katika usajili wa kudumu na vimeshiriki uchaguzi mkuu ni vyama 22 hivyo watu watambue chama cha TPP kilishafutwa kutokana na kukiuka kwa taratibu za ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Nyahoza amesema kuwa watu wote wanaotumia vyama ambavyo usajili wake ulishafutwa kwa mamlaka ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa watatachukuliwa hatua.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post