Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA_JINSI MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI ULIVYOAGWA JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais, Dk. Bilal akielekea kutoa heshima za mwisho kwa Kombani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar Balozi, Seif Ally Idd, akitoa heshima za mwisho.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akiuaga mwili wa marehemu Kombani.
Anne Makinda akitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa Celina Kombani.
Mama Maria Nyerere akiwa mbele ya jeneza.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva, akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza.

Kamanda Maalum wa Kanda ya kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova naye alikuwepo.
Huyu ni Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fenala Mkangala.
Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipita mbele ya jeneza.

Hapa ni Waziri wa Uchukuzi, Samweli Sitta akionyesha masikitiko yake.
Anne Makinda (katikati) akiwa na Mama Maria Nyerere (kushoto) katika viwanja vya Karimjee kabla ya kuuaga mwili wa Kombani.
Gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemui.
Jeneza la mwili wa Kombani likiwa katika viwanja vya Karimjee.
Msanii wa filamu Wema Sepetu akiuaga mwili wa Kombani.
Waombolezaji wakielekea kwenye jeneza.
Hali ilivyokuwa viwanjani hapo.
Mmoja wa wanafamilia akilia kwa uchungu.
Mume wa marehemu Kombani (katikati) akiwa na simanzi.Celina Kombani enzi za uhai wake.








Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa waziri wa nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma Mh Celina Kombani zoezi lililofanyika viwanja vya Kareemje jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa maziko.




Mara baada ya mwili huo kuwasili katika viwanja hivyo mchungaji Wilfred Mmari ameongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu kabla ya makundi mbalimbali kutoa salaam zao za rambirambi.

Akisoma salamu za serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama mbali na kueleza uadilifu uliotukuka wa marehemu Kombani amesema ndani ya serikali ameacha pengo huku mwakilishi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar naye akitoa salaam.

Naye spika wa bunge anayemaliza muda wake Mh Anne Makinda akitoa salaam kwa niaba ya ofisi ya bunge amewataka watumishi wa umma kutumia msiba huo kutafakari na kurekebisha maisha yao kwa kuwa na upendo na kuwatumikia wananchi kwa kutoa huduma bora.

Baadhi ya mawaziri wenzake na wabunge waliojitokeza kuuaga mwili huo wamemwelezea marehemu Kombani namna alivyokuwa mwalimu wao kila mara walipotaka ushauri wake ndani na nje ya bunge.

Mbali na makamu wa rais baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria zoezi hilo ni pamoja na mawaziri, wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, mama Maria Nyerere na mama Salma Kikwete.

Akisoma wasifu wa marehemu mwakilishi wa serikali amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya kongosho iliyokuwa imeathiri ini lake na alizaliwa june 19 1959 na kufarifariki dunia septemba 24 mwaka huu katika hospitali ya Apollo nchini India na mwili wake unatarajiwa kuzikwa sept 29 mkoani Morogoro na ameacha mume,watoto watano na wajukuu wanne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com