KARANI WA MAHAKAMA ATUPWA JELA BAADA YA KUGOMA KUSAINI CHETI CHA NDOA...



Kim Davies aliyekataa kusaini cheti cha ndoa Kentucky


Jaji mmoja nchini Marekani, ameagiza afisa mmoja wa serikali katika jimbo la Kentucky, kufungwa jela, baada ya kukataa kutekeleza agizo la mahakama la kutoa cheti rasmi cha ndoa, kwa wapenzi wawili wa jinsia moja.

Kim Davies amesema imani yake kama Mkristo, haimruhusu kusaini cheti kama hicho. Ndoa ya jinsia moja ilihalalishwa nchini Marekani Juni mwaka huu.

Umauzi huo wa Davis, wa kutosaini cheti hicho umepokelewa kwa hisia tofauti.

Kuna baadhi ya wale wanaomuona kama shujaa huku wengine wakisema ni msaliti.

Tofauti za imani

Davis ambaye ni karani wa mahakama, alikataa kutoa cheti hicho, kwa wanandoa hao katika kaunti ya Rowan iliyoko Kentucky.

Afisa huyo ambaye alichaguliwa na raia amesema, kitendo hicho kinakiuka maadili ya kidini.

Davis sasa ametupwa jela na jaji huyo kwa kudharau mahakama.

Amesema alikuwa amekula kiapo cha kuwa ofisini na viapo vina maana nyingi.

Watu wanaoshabikia ndoa ya jinsia moja, walikusanyika nje ya mahakama, wakiimba kuwa mapenzi imeshinda na kusema kuwa sasa wanafuraha kwa sababu wanaweza kufunga ndoa.

Lakini kwa upande wake Kim Davis amepata uungwaji mkono kutoka kwa Wakristo wahafidina na baadhi ya wagombea wa urais wa chama cha Republican, ambao wanasema kuwa Davis amehukumiwa jela kwa kufuata imani zake.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post