Punda huyo akiwa ameuawa na kuchomwa moto na wananchi baada ya tukio hilo.
Maajabu!! Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto Bosco Daudi mwenye umri wa miezi 5 amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya Punda kumng’ata na kuanza kukimbia naye katika soko la Lumambo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza na Malunde1 Blog mama mzazi wa mtoto huyo Dafroza John (23) mkazi wa mtaa wa Shunu wilayani Kahama amesema mwanaye alichukuliwa na punda huyo alipokuwa amemweka chini wakati anawahudumia wateja katika soko hilo.
Mama wa mtoto huyo Dafroza John akiwa amemshikilia mwanae hospitalini hapo.
Dafroza ameongeza kuwa baada ya mwanaye kuchukuliwa na punda huyo alianza kupiga kelele za kuomba msaada na ndipo wasamaria wema wakajitokeza na kisha kumfukuza kwa umbali wa zaidi ya mita 100 hadi alipomwachilia na kukimbia.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Sudi Tomas ameiambia Malunde1 Blog kuwa baada ya Punda huyo kumwachilia mtoto huyo waliamua kumfukuza hadi walipomkamata na kisha kuanza kumshambulia kwa mawe hadi kumuua kabla ya kumchoma moto.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya watoto katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama Bundala Boniface amesema mtoto huyo amepata majeraha katika sehemu ya kifua na bado wanaendelea kumpatia matibabu.

Hili ni tukio la kwanza la aina yake ambalo limezua sintofahamu miongoni wa wakazi wa manispaa ya Kahama kwa mnyama Punda kumchukua mtoto kwa mdomo wake na kisha kuanza kukimbia naye.