Mtu wangu wa nguvu bado Malunde1 blog inakusogezea uzuri wa dunia, huenda umewahi kutembelea vivutio vingi vya utalii duniani lakini huenda hukuwahi kubahatika kufika wala kusikia kuhusu maziwa haya mazuri ya kuvutia yenye muonekano wa umbo la moyo au kopa. Hii ni stori ambayo nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, hivyo nikaona sio vibaya September 22 nikakusogezea karibu yako Top 10 ya maziwa yenye muonekano wa moyo duniani. Chanzo cha hii stori ni World – World Top Top. Huu ni muonekano wake kwa juu
1- Ziwa Shimshal – Pakistan
Hili ni ziwa lenye umbo la moyo na lipo katika bonde la Hunza Pakistan
2- Gaislacher See – Austria
Hili lipo Australia katika mlima Gaislachkogel
3- Heart Lake – Canada
Hili lipo Canada pembeni limezunguukwa na maua mazuri lipo karibu na Ompah, Ontario
4- The Coeur de Voh – New Caledonia
Muonekano wake kwa juu umepambwa na maua yanayoelea juu ya maji.
5- Crater – Uturuki
Crater lipo Uturuki mpakani mwa Cappadocia
6- Heart Lake – Urusi
Lipo Urusi na inatajwa kama unataka kuona muonekano wake kwa juu utatumia masaa 5 kupanda kilele cha mlima Cherskogo
7- Hili ni bwawa lipo USA (Marekani)
Bwawa hili pia lipo karibu na Strongsville Ohio
8- Chicago – Colorado – USA
Sio lazima ulitazame kwa juu ili ujue kama lina umbo la moyo hata kwa chini ukitazama Chicago linaonekana kuwa na umbo hilo.
9- Aral Sea – Kazakhstan
Sehemu ya Kusini ya Aral Sea ndio inaonyesha muonekano wa umbo la moyo
10- Eros – India
Ukiwa unaelekea kilele cha mlima Chembra ni rahisi kuona muonekano wa Eros.
Social Plugin