Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa Haya!! AZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KULEWA POMBE




Mtu mmoja nchini India amefariki baada ya wafanyAkazi wa ujenzi ambao hawakumuona katika shimo hivyo kumzika akiwa hai.

Kisa hicho kilitokea katika wilaya ya Katani katika mji wa jimbo la Pradesh.

Maafisa wa polisi wamesema kwamba mtu huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa amelewa alipoanguka katika shimo hilo.

Watu wawili akiwemo dereva mmoja wa lori ambaye alimwaga changarawe hiyo wamekamatwa.

Kisa hicho kilibainika baada ya wanakijiji kuona mkono uliokuwa umejitokeza chini ya changarawe hiyo.

Mtu huyo anaaminika kuelekea nyumbani kutoka kijiji kimoja kabla ya kuanguka katika shimo hilo.

Mamlaka ya taifa hilo imeagiza kufanyika kwa uchunguzi na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaopatikana na hatia.

Via>>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com