Zaidi ya wafungwa 4000 wameondolewa katika gereza la Pollsmoor Prison lililopo Afrika Kusini baada ya panya kuvamia gereza hilo na kusababisha vifo vya wafungwa wawili.
Mmoja wa viongozi wa gereza hilo Manelisi Wolela, amesema wamelazimika kuwahamisha wafungwa hao hadi pale watakapowaangamiza panya hao.
Amesema panya hao wamesababisha magonjwa kwa wafungwa na kuleta usumbuufu mkubwa.
Gereza la Pollsmoor pia liliwahi kutumiwa na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo.
Mandela alihamishwa kutoka jela ya Robben Island na kupelekwa Pollsmoor mwaka 1982.
Social Plugin