MATOKEO YA SIMBA Vs KAGERA SUGAR NA MECHI ZINGINE ZA LIGI KUU LEO JUMAPILI
Sunday, September 20, 2015
Klabu ya Simba SC September 20 imerejea katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaamkumkaribisha mgeni wake Kagera Sugar kutoka Bukoba, Simba ambayo imerejea kutokea Tanga ambapo ilicheza mechi zake mbili za awali katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo mechi ya kwanza ilicheza dhidi ya African Sports ya pili na Mgambo Shooting.
Simba imerejea kucheza mechi yake ya tatu uwanja wa Taifa Dar Es Salaamhuku nahodha wao Mussa Hassan Mgosi akiwa jukwaani, Simba ambayo hadi sasa imecheza mechi mbili na kushinda zote. September 20 katika mechi dhidi ya Kagera Sugar, Simba imeibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-1.
Magoli ya Simba yalifungwa kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza dakika ya 30 baada ya kutumia vizuri krosi kutoka kwa Awadhi Juma. Kiizaalipachika magoli mengine mawili dakika ya 46 na 92 ya mchezo, huku Kagera Sugarwakiambulia goli moja peke lililofungwa na Mubaraka Yusuph dakika ya 60.
Haya ni matokeo ya Mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa September 20
Mwadui FC 0 – 1 Azam FC
Mtibwa Sugar 2 – 1 Ndanda FC
Coastal Union 0 – 0 Toto Africans
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin